MichezoPilipili FmPilipili FM News

Timu Za Zoo Fc Na Nakumatt Zarudishwa Ligini.

Mahakama ya rufaa nchini imebatilisha uamuzi uliotolewa na mahakama kuu jijini Nairobi wakuziondoa timu za Zoo fc na Nakumatt kwenye ligi kuu ya humu nchini.

Timu hizo mbili zilidondoshwa nje ya ligi hio wiki iliyopita baada ya mahakama kuu kupitia jaji John Mativo kuelezea kuwa zilikua kwenye ligi kinyume cha sheria kwani zilipandishwa daraja katika hali ya kutatanisha.

Mahakama kuu ikaagiza timu hizo ziondolewe ligini na ligi ibakizwe na timu 16 badala ya 18 kama shirikisho la soka nchini FKF lilivyopendekeza.

Lakini FKF kupitia rais wa shirikisho hilo Nick Mwendwa ilikinzana na uamuzi huo na kupeleka rufaa yake katika mahakama ya rufaa ambapo maombi yao yamekubaliwa kwenye mahakama hio na sasa ni afueni kwa timu za zoo fc na nakumatt kwani zimepata ithibati ya kushiriki ligi kuu ya humu nchini.

Kesi hii inajiri baada ya aliyekua rais wa shirikisho la soka nchini kuwasilisha kesi mahakamani kupinga kuongezwa kwa timu kutoka 16 hadi 18.

 

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker