MichezoMilele FmSwahili

Nakummat FC na Zoo Kericho kurejea kwenye ligi kuu humu nchini

Vilabu vya Nakumatt Fc NA Zoo Kericho vinarejea kwenye ligi kuu humu nchini , hii ni kufuatia uamuzi uliotolewa na mahakama ya rufaa mapema hii leo.
Pande hizo mbili pamoja na shirikisho la kandanda FKF ziliwasilisha kesi mbele ya mahakama hiyo kupinga uamuzi kuondolewa kwao kwenye ligi kuu, hii ni baada ya mahakama ya juu kuamuru kwamba ligi kuu inapaswa kushirikisha vilabu 16 na sio 18 ilivyoamuliwa na mahakama ya michezo SDT mapema mwaka huu.
Kocha wa Nakumatt Antony Mwangi amefurahia uamuzi huo . Zoo na Nakumatt waliopandishwa ngazi baada ya idadi ya timu shiriki kwenye ligi kuongezwa hadi 18 hawajashiriki raundi tatu zilizopita za ligi kuu ya KPL.

Show More

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker