MakalaMilele FmSwahili

Rais Kenyatta aiomba mahakama ya juu kutupilia mbali kesi inayopinga ushindi wake

Rais Uhuru Kenyatta ameiomba mahakama ya juu kutupilia mbali kesi ya kupinga ushindi wake. Kupitia wakili Ahmednassir Abdullahi,rais Kenyatta amesema alichaguliwa na wakenya zaidi ya milioni nane na kuitaja kesi hiyo kama isiyo na msingi. Ametaja madai ya mpinzani wake Raila Odinga kwamba lishirikiana na IEBC kuiba kura kama propaganda. Amesisitiza alimshinda mpinzani wake kwa wingi wa kura.

Show More

Related Articles