HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Maafa ya Kipindupindu : Watu 3 wathibitishwa kufariki Kisumu wakiwemo wafungwa

Watu watatu wameripotiwa kufariki katika gereza la Kodiaga kaunti ya Kisumu, kufuatia mkurupuko wa maradhi ya Kipindupindu katika eneo hilo.
Waliofariki ni wafungwa wawili na mwanakijiji mmoja ambaye anaishi karibu na gereza hilo.
Wafungwa wengine ishirini na wanne pia bado wamelezwa katika zahanati ya gereza hilo, watano katika yao wakiwa katika hali mahututi.
Na huku haya yakijiri, serikali ya kaunti ya Machakos pia imefungwa mikahawa kumi na saba ambayo imekiuka sheria ya afya katika kaunti hiyo.

Show More

Related Articles