Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wagombeaji wakuu wa urais walenga ngome zao kipindi hiki

Kufuatia takwimu zilizotolewa na mashirika mawili ya utafiti kuhusu kura ya maoni jumapili iliyopita, wakenya wengi wamepata dhana kwamba uchaguzi wa mwaka huu huenda ukaingia kwenye duru ya pili .
Hii ni baada ya tafiti hizo kuashiria kwamba huenda kukakosekana mwaniaji atakayepata asilimia 50 na zaidi kama ilivyoratibiwa kwenye katiba.

Anders Ihachi amezungumza na mkurugenzi wa shirika la utafiti la Trends and Insights for Africa, Tifa, Maggie Ireri ambaye anasisitiza kwamba mkondo wa mambo utabainika bayana katika siku zilizosalia kabla ya debe.

Show More

Related Articles