HabariMilele FmSwahili

Wazee kutoka jamii za Kamba na Gema zamuunga mkono Mike Sonko kwa azma yake ya kuwania ugavana

Wazee kutoka jamii za Kamba na Gema wametangaza kumuunga mkono seneta Mike Sonko katika azma yake ya kuwania ugavana hapa Nairobi. Wakizungumza katika mkutano ambao pia ulihudhuriwa na mgombea mwenza wa Sonko Paul Igathe wazee hao wanasema wana imani utawala wa Sonko utaleta mafanikio makubwa jijini Nairobi. Igathe kwa upande wake amewahakikishia kuwa agenda yake kwa ajili ya jiji hili itasaidia kuibadili.

Show More

Related Articles