HabariMilele FmSwahili

Kesi ya ufisadi dhidi ya Peter Mangiti kuendelea

Kesi ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa katibu katika wizara ya ugatuzi Peter Mangiti itaendelea. Hii ni baada ya mahakama kuu kutupilia ombi alilowailisha kutaka kesi ambapo anahusishwa na sakata ya shilingi milioni 791 za NYS kutupiliwa mbali kwa msingi kwamba alikuwa anaandamwa bila ushahidi wowote. Jaji wa mahakama ya kupambana na ufisadi Hedwig Ong’udi ameamua kwamba kesi hiyo sharti iskizwe kabla ya kubaini endapo kuna ushahidi au la. Mangiti anadaiwa kulipa milioni 47.6 kwa moja wapo ya kampuni zilizopokea milioni 791 zilizoibwa kutoka kwa NYS.

Show More

Related Articles