HabariMilele FmSwahili

IEBC kutii sheria katika utangazaji wa matokeo ya kura

Tume ya uchaguzi na mipaka sasa inasema itafuata sheria katika kutagaza matokeo yote ya upigaji kura. Afisa mkuu mtendaji Ezra Chiloba anasema IEBC haitatangaza matokeo ya maeneo bunge katika kituo kikuu cha kujumlisha kura, bali yatatangazwa na makarani wa vituo hivyo. Chiloba akikutana na washika dau wa vyombo vya habari kaitka ukumbi wa Bomas amesema kuna vituo 338 vya kujumlisha matokeo ambavyo vina mfumo wa kuhakikisha matokeo hayo yananakiliwa kwa wakati kupitia mitandao.

Show More

Related Articles