HabariMilele FmSwahili

Raila Odinga aahidi kuwahudumia wakenya wote bila ubaguzi akichaguliwa Agosti nane

Kinara wa NASA Raila Odinga anahidi kuwahudumia wakenya wote bbila ubaguzi iwapo atachaguliwa Agosti nane. Akiwahutubia wenyeji wa Tharaka Nithi katika ziara ya kujipigia debe, Raila amesema NASA itahakikisha imeunganisha jamii zote. Amekanusha madai eneo la mlima Kenya ni ngome ya Jubilee akiwaomba wenyeji kumpigia kura kuliongoza taifa. Kinara wa Ford Kenya Moses Wetangula anayeandamana na Raila amewarai wakenya kufanya uamzi wa busara ifikiapo Agosti nane na kuwachagua viongozi watakaojali maslahi yao. Wana NASA wameratibiwa kuhutubia mkutano mkuu huko Laare kaunti ya Meru alasiri hii.

Show More

Related Articles