HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta: Sijutii kutohudhuria mdahalo wa wagombea urais

Rais Uhuru Kenyatta anasema hajutii kutohudhuria mdahalo wa wagombea urais jana. Akiwahutubia wenyeji wa Othaya kaunti ya Nyeri, rais Kenyatta ameshtumu vyombo vya habari kwa kueneza propaganda dhidi ya hatua yake kususia mdahalo huo akisema lengo lake ni kuzungumza na wakenya moja kwa moja mashinani. Amemshutumu kinara wa NASA Raila Odinga kwa kutumia mdahalo huo kuwahadaa wakenya.Rais ambaye pia amewahutubia wenyeji wa Tetu ameshtumu upinzani kwa kueneza siasa za propaganda akitaja hatua hiyo kama ishara ya kukosa ajenda kwa wakenya.Kwa upande wake naibu rais William Ruto amepuuza madai serikali imewatelekeza wananchi wa magharibi mwa Kenya. Akiongea huko Kakamega,naibu rais amesema serikali imetekeleza miradi kadhaa eneo hilo.

Show More

Related Articles