HabariMilele FmSwahili

Karatasi za kupiga kura ya urais kuwasili nchini mwishoni mwa wiki hii

Karatasi za kupigia kura ya urais zitawasili nchini kuanzia mwisho wa wiki hii. Tume ya uchaguzi imetoa hakikisho hilo ilipokutana na viongozi wa dini pamoja na wazee wa jamii kuwaelezea mikakati ya uchaguzi. Kamishna Dkt Paul Kurgat anasema wanatarajia karatasi zote zitakua nchini kufikia Agosti tarehe tatu. Wakati huo huo IEBC imewataka maafisa wa usalama kutekeleza majukumu yao kuambatana na sheria wakati wa uchaguzi. Viongozi hao wa kiini walielezea kuridhishwa kwao na mikakati iliyowekwa na IEBC kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzui huru na wazi.

Show More

Related Articles