HabariMilele FmSwahili

Joel Kitili awaomba wakenya kuwa na imani kwa idara ya polisi wakati huu wa uchaguzi

Naibu inspekta wa polisi Joel Kitili amewaomba wakenya kuwa na imani kwa idara ya polisi wakati huu inapojiandaa kuimarisha usalama kabla na baada ya uchaguzi mkuu. Kitili anasema polisi wote walikula kiapo cha kulinda maisha ya wakenya wote bila ubaguzi wakati wowote wanapohitajika. Akiongea huko Isbania kaunti ya Migori kwenye hafla ya mazishi ya aliyekua kamishena wa polisi Thomas Turuka, Kitili amesema usalama wa taifa ni jukumu la kila mmoja huku akiwoanya wnaasiasa dhidi ya kueneza semi za chuki. Amewaomba wakenya wote kudumisha amani kabla na baada ya uchaguzi kwa ajili ya umoja wa taifa.

Show More

Related Articles