HabariPilipili FmPilipili FM News

Mbunge Wa Mwatate Awasuta Wapinzani Wake

Mbunge wa Mwatate katika kaunti ya Taita Taveta Andrew Mwadime amewasuta baadhi wapinzani wake kwa kuwahadaa wakazi wa eneo hilo kuhusiana na baadhi ya miradi aliyoanzisha yeye binafsi.

Mwadime ameitaja hatua hiyo kuwa njama ya viongozi wa kisiasa kujitafutia umaarufu, akisema viongozi hao  wamekosa malengo ya kuendeleza eneo hilo, na kuwataka wakaazi kujiepusha na propaganda zinazoenezwa dhidi yake.

Mwadime ameyaongea haya mjini Mwatate kwenye hafla ya kufungua madarasa mapya, yaliojengwa kupitia hazina ya CDF kwenye shule ya msingi ya kitivo.

Show More

Related Articles