HabariPilipili FmPilipili FM News

Waziri Balala Akanusha Kushuka Kwa Utalii.

Waziri wa utalii Najib Balala amepuuzilia mbali madai kuwa sekta ya Utalii imeanza  kushuhudia upungufu wa idadi ya wageni wakati huu ambapo taifa linajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa agosti.

Akiongea na meza yetu ya habari Balala amehoji kuwa sekta hiyo haijapata tishio lolote la kupungua kwa idadi ya wageni kutokana na msimu wa uchaguzi.

Aidha waziri Balala amesisitiza umuhimu wa taifa la Kenya kudumisha amani kuona kuwa sekta ya utalii haiathiriki kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Utalii ni sekta ya pili katika kuletea taifa la Kenya pesa za kigeni baada ya kilimo.

Show More

Related Articles