HabariPilipili FmPilipili FM News

IEBC Yatakiwa Kuweka Wazi Mipango Yake Ya Maandalizi Ya Uchaguzi Nchini.

IEBC Imetakiwa kuweka wazi  mipango yake ya maandalizi ya uchagizi ili  kuondoa hofu kuhusiana na  sheria npamoja na  mikakati yake  ya kusimamia uchaguzi nchini.

Hii ni kauli ya Zaidi ya mashirika ishirini yasiokuwa ya serikali yakiishinikiza tume ya  IEBC,  yakisema lazima  iweke wazi kila hatua wanayopanga kwa wananchi.

Yakiongea na waandishi wa habari hapa mjini Mombasa kupitia Mkurugenzi wa shirika la KECOSKE  Philis Mwema,  pia yameitaka idara ya usalama kuwahakikishia wananchi usalama wa kutosha huku Idara ya usalama ikionywa kuweka hadharani maandalizi yao  ya kupambana na vurugu, Mashirika hayo yakisema kitendo hicho kinazidi kuwatia wananchi hofu ya kuzuka kwa vurugu.

Philis Mwema pia amewataka wanasiasa kuheshimu uamuzi wa wakenya kwenye matokeo ya uchaguzi na kuongeza kwamba yeyote ambaye hata ridhishwa na matokeo hayo afate jinsi sheria  inaruhusu kikatiba.

Show More

Related Articles