HabariMilele FmSwahili

Mfungwa afariki kutokana na kipindupindu katika gereza la Kodiaga Kisumu

Mfungwa moja katika gereza la Kodiaga kaunti ya Kisumu amefariki na wengine 35 kulazwa hospitalini baada ya kuugua kipindipindu. Kamanda wa magereza eneo la Nyanza, Amos Misik anasema 36 hao walianza kuonyesha dalili za ugonjwa huo jana kabla ya kulazwa hospitalini kwa matibabu. Haya yanajiri huku serikali ya Machakos ikifunga zaidi ya hoteli 17 eneo bunge la Kangundo baada ya kuripotiwa mkurupuko wa kipindupindu eneo hilo.

Show More

Related Articles