HabariMilele FmSwahili

Mchezaji wa raga klabu ya KCB James Kilonzo auwawa

Mchezaji wa raga klabu ya KCB James Kilonzo ameaga dunia.inakisiwa kwamba  Kilonzo alirushwa risasi na watu wasiojulikana katika duka la Mpesa maeneo ya kasarani hapa jijini Nairobi.

Kilonzo alikuwa miongoni mwa kikosi cha KCB kilichosafiri Afrika Kusini kwa kambi ya siku kumi baada ya kushinda kombe la Enterprise na pia kuibuka mabingwa wa ligi kuu ya raga humu nchini mwezi mei mwaka huu.

Hapo awali alihudumu na klabu ya Catholic Monks.

Show More

Related Articles