HabariPilipili FmPilipili FM News

Gavana Kingi Ahimiza Wafanyikazi Wa Viwanda Kupigia Kura NASA.

Gavana wa Kaunti ya Kilifi Amason Kingi amewataka wafanyikazi wa viwandani katika kaunti hiyo  kupigia kura mrengo wa NASA ili kujikomboa kutokana  na mikakati mibovu ya  Serikali ya kitaifa ambayo  imesababisha kupanda kwa gharama ya maisha hapa nchini.

Akizungumza na wafanyikazi takriban 500 wa viwanda vya EPZ pamoja na Umoja Rubber eneo la Kikambala Kingi amedai kuwa wafanyikazi wengi bado  wanapokea mishahara duni licha ya  majukumu ya wizara ya Leba kuwa  mikononi mwa serikali kuu.

Hata hivyo Kingi ameongeza kuwa miundo msingi duni ya serikali ya kitaifa ndio inapelekea  utekelezaji wa mishahara duni miongoni mwa  wafanyikazi licha ya gharama ya maisha kushuhudiwa kupanda kila siku.

 

Aidha  Kingi amewataka wafanyikazi hao pamoja na wakazi wote wa Pwani wajitokeza kikamilifu na waupigie kura muungano wa NASA iwapo wanataka mabadiliko ya sheria za Leba.

 

 

Show More

Related Articles