HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwalimu Mkuu Wa Shule Ya St Augustine Mombasa Agizwa Kufika Mahakamani.

Mahakama kuu mjini Mombasa imetoa agizo la kufika mahakamani kwa jamaa watano akiwemo mwalimu  mkuu wa shule ya msingi ya st Augustine kujibu mashtaka ya mauaji ya mwanafunzi wa shule hiyo ambaye alikanyagwa na basi la shule mapema wiki iliyopita.

Watano hao ambao ni Kesi Sara ambaye ni mwalimu mkuu wa shule hiyo, Venant mwaliko dereva wa basi la shule Vald Mbadi fundi wa gari hilo,charo kazungu msaidizi wa dereva na Abednego fundi mmoja wa wafanyikazi wa shule hio wameagizwa kufika mbele ya mahakama  siku ya jumatano kusomewa mashtaka dhidi yao.

Akiwasilisha ombi hilo mbele ya mahakama naibu mkuu wa mkurugezi wa mashtaka ya umma Alexander Muteti amesema wamechukua hatua hio ili kuwafahamisha jamaa hao wafike mahakamani

Wakati huohuo Muteti amesema kigezo cha washukiwa hao kutojua kama walihitajika mahakamani leo ndio sababu wameomba waagizwe kufika mahakamani wala sikukamatwa.

Hata hivyo mashirika ya kijamii yamelaumu afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kwa kile wanachodai kucheleweshwa kwa kesi hio.

Jamaa hao kulingana na mahakama wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ambapo inaarifiwa mnamo tarehe 21 ya mwezi huu kwa pamoja wanadaiwa kuhusika kwa mauaji ya mwanafunzi wa chekechea wa shule hio.

Show More

Related Articles