HabariMilele FmSwahili

Peter Kenneth apuuza wito wa Rais kujiondoa katika kinyanganyiro cha ugavana Nairobi

Muaniaji ugavana kaunti ya Nairobi Peter Kennet amepuuza wito wa Rais Uhuru Kenyatta kwake kujiondoa katika kinyanganyiro na kumuunga mkono seneta Mike Sonko wa Jubilee. Akijibu wito wa rais Kenyatta alipoongoza kampeni ya Jubilee hapa Nairobi wikendi iliyopita, Kenneth amemtaka rais Kenyatta kuwaruhusu wakazi wa Nairobi kumchagua mgombea wanayempenda bila kushawishiwa. Akizungumza katika katika mtaa wa Karen Kenneth ameapa kugatua huduma mashinani iwapo atachaguliwa gavana Epya wa Nairobi. Pia amewataja Sonko na gavana dkt evans Kidero kama waliofeli na hawawezi kutatua matatizo yanayowakumba wakazi.

Show More

Related Articles