BurudaniPilipili FmPilipili FM News

Ohms Law Apagawisha Mashabiki Tononoka.

Huku msimu wa siasa ukiendelea kupamba moto wasanii nao hawajaachwa nyuma kwani hii ndio season yao yakuvuna mihela tele.

Msanii wa hivi punde kupagawisha wafuasi wa kisisa katika mkutano wa hadhara ni Ohms Law Montana mwana hip hop ambaye ni mmoja ya wasanii ambao wanakipaji kikubwa hususani akiwa kwa stage hua anaimiliki nakuleta mshawasha kwa mafans wake.

Ohms katika mkutano wa hadhara eneo la Tononoka wakati wa mkutano wa mwaniajai wa ugavana kaunti ya Mombasa Hassan Sarai aliwafanya mashabiki kusahau wako katika mkutano wa kisisa na kwa kutoa burudani safi lilomfanya mwanasiasa Sarai kuacha kiti chake na kuimba pamoja na Omhs kwenye jukwaa.

Hali hii imedhihirisha wazi umuhimu wa wasanii waka huu lakini swali ni je wanasiasa hawa watakapoingia kwenye nyadhifa hizo watawakumbuka wasanii hawa?

Wengine ambao wanaonekana kufaidi kipindi hiki ni P Day, Papa, Susumila, Dazlah ,Frankie D Fat S, Ally B na wengine wengi.

Wenyewe wanasema wako high season na kwa kusema kweli wako kwa high season kwani wako viwanjani kutafuta.

Show More

Related Articles