HabariPilipili FmPilipili FM News

Onyo La Mwadeghu Kwa Wakaazi Wa Taita.

Mwaniaji wa ugavana kaunti ya TaitaTaveta kupitia chama cha ODM Thomas Mwadeghu amewataka wakazi wa kaunti hiyo  kukataa kuhadaiwa na viongozi wanaotafuta nyadhfa mbalimbali katika kaunti hiyo.

Mwadeghu amesema kaunti hiyo inahitaji viongozi  wenye maono ya kuhakikisha matatizo yanayoshuhudiwa eneo hilo yamekabiliwa vilivyo, na wala sio viongozi wa kujinufaisha kibinafsi.

Amewarai wananchi kutumia muda uliosalia kabla ya uchaguzi kuwakagua viongozi wanaotafuta uongozi akiongeza kuwa yeye binafsi atakubali matokeo ya uchaguzi mkuu wa agosti.

Show More

Related Articles