HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakuu Wa Shule Ya St Augustine Mombasa Kuonja Makali Ya Sheria.

Watu watano akiwemo mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya St.Augustine mjini  Mombasa wanatarajiwa  kufikishwa mahakamani hii leo kufuatia kifo cha mwanafunzi wa shule hiyo juma lililopita.

Mwanafunzi huyo wa chekechea alifariki baada a kukanyagwa na basi la shule hiyo, pale alipo jaribu kuchukua chupa yake ya maji , iliyoanguka kupitia shimo lililokuwepo kwenye sehemu ya chini ya basi hilo.

Alexander Muteti ambaye ni msaidizi katika afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kaunti ya Mombasa, anasema tayari wamepokea faili ya mashtaka kutoka kwa maafisa wa polisi kuhusiana na tukio hilo.

Kulingana na polisi shimo hilo lilikuwa limezibwa na kifaa dhaifu, ishara tosha kwamba usimamizi wa shule ulitambua kuwepo kwake bila kuchukua hatua zifaazo.

Shallim Massilla ni nyanyake mtoto huyo akiongea baada ya ajali hiyo.

Show More

Related Articles