HabariPilipili FmPilipili FM News

IEBC Yatoa Makataa Kwa Vyama Vya Kisiasa.

Vyama vya kisiasa vimepewa mda wa hadi leo kuwasilisha orodha ya mawakala watakakua katika vituo vya kura siku ya uchaguzi.

IEBC imesema kulingana na sheria za uchaguzi vyama vinapaswa  kuwasilisha orodha hiyo siku 14 kabla ya uchaguzi mkuu kuandaliwa.

Kupitia taarifa kwenye mtandao wake wa twitter,IEBC imeeleza kuwa kila chama kitawakilishwa na wakala mmoja katika kituo cha kitaifa cha kujumlisha matokeo,mawakala 47 ambao watakuwa katika kila kituo cha kaunti cha kujumlisha matokeo, na wale wayakaokua katika vituo vya kupigia kura.

Show More

Related Articles