HabariMilele FmSwahili

Mathew Lempurkel kufikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka ya uchochezi

Mbunge wa Laikipia kaskazini Mathew Lempurkel anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo kujibu mashtaka ya uchochezi.Lempurkel alikamatwa na polisi siku ya jumamosi huko Nanyuki kaunti ya Laikipia. Anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea jamii za wafugaji ambapo anadaiwa kuwambia wananchi wasio wenyeji wa Laikipia kwamba wataondolewa kwa lazima iwapo NASA itashinda uchaguzi wa Agosti nane. Amekua akizuliwa na polisi huko Narumoru tangu siku ya Jumamosi alipokamatwa. Kamanda wa polisi huko Laikipia Simon Kipkeu anasema Lempurkel alinaswa katika kanda za vedeo akiapa kuwafurusha wasio wenyeji wa Laikipia.

Show More

Related Articles