HabariMilele FmSwahili

Kenya na Tanzania zakubaliana kuondoa vikwazo vya uagizaji na uuzaji bidhaa

Kenya na Tanzania zimekubaliana kuondoa vikwazo vya uagizaji na uuzaji bidhaa. Maafikiano hayo sasa yatapelekea Kenya kuondoa ushuru unaokatwa bidhaa za unga wa ngano na gesi huku Tanzania ikiondoa ushuru unaokatwa maziwa na sigara. Haya yameafikiwa baada ya mazungumzo baina ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na mwenzake wa Tanzania John Pombe Magufuli kupitia taarifa iliosomwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga hapa Nairobi. Aidha nchi hizi mbili zimekubaliana kuunda kamati ya pamoja itakayojadili na kutoa mapendekezo ya kumaliza migogoro ambayo imekua ikishuhudiwa baina ya Kenya na Tanzania

Show More

Related Articles