HabariK24 TvSwahiliVideos

Wachunguzi wa kimataifa wa AU wapuuzilia mbali hofu ya kuzuka kwa ghasia baada ya uchaguzi

Wachunguzi wa kimataifa wa umoja wa Afrika, AU, wakiongozwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, hii Jumamosi wameelezea matumaini yao kwamba Kenya iko tayari kuuandaa uchaguzi wa haki na huru siku 16 kutoka sasa pasipo hofu ya kuzuka kwa machafuko ya aina yoyote.
Mbeki ambaye hapo Ijumaa alikutana na wadau kadha wakiwemo, kaimu waziri wa usalama Dkt. Fred Matiang’i, tume huru ya uchaguzi na mipaka,IEBC pamoja na mabalozi wa bara amesema kwamba Kenya ni taifa muhimu sana barani Afrika, hivyo basi hawataruhusu ichukuwe mkondo wa mwaka 2007/8.
Wachunguzi zaidi ya mia moja wa kimataifa wanatarajiwa kuwasili humu nchini kabla siku ya uchaguzi Agosti nane.

 

Show More

Related Articles