HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta aahidi kufungua mpaka wa Kenya na Somalia

Rais Uhuru Kenyatta amehaidi kufungua mpaka wa Kenya na Somalia ili kuimarisha biashara baina ya mataifa ya Kenya na Somalia. Akiwahutubia wenyeji wa Mandera katika uwanja wa Moi mjini Mandera, rais Kenyatta amesema serikali inaweka mikakati wa kuimarisha usalama kaunti hiyo kabla ya kufunguliwa kwa mpaka kuwezesha biashara baina ya mataifa hayo mawili. Rais anayendamana na naibu wake katika ziara ya kujipigia debe kaunti hiyo amesema lengo la serikali ya Jubilee ni kuinua uchumi wa wananchi kupitia biashara.

Show More

Related Articles