HabariMilele FmSwahili

Mbunge wa Laikipia Mathew Lempurkel atiwa mbaroni

Mbunge wa Laikipia North Mathew Lempurkel amekamatwa. Mbunge huyo ametiwa mbaroni na maafisa wa idara ya ujasusi mjini Nanyuki kaunti ya Laikipia. Anatarajiwa kuhojiwa na polisi huko Narumoru kuhusiana na madai ya uchochezi. Kukamatwa kwake kunajiri siku moja tu baada ya mbunge wa suna east Junnet Mohammed kukamatwa na kuhojiwa kuhusiana na madai ya uchochezi huko Homa bay.

Show More

Related Articles