HabariMilele FmSwahili

Kenya inakabila 44

Kenya ina kabila la 44. Hii ni baada ya rais Uhuru Kenyatta kuchapisha katika gazeti la serikali kutambuliwa kwa wakenya wa asili ya kihindu kama kabila la 44. Huku akirejelea katiba inayompa mamlaka ya kutambua kuafikia uamzi huo,rais Kenyatta amesifia wakenya wa asili hiyo akiwataja kama ambao wamechangia katika ukuaji wa taifa hili. Hatua hiyo inajiri miezi michache baada ya rais Kenyatta kuwatambua wananchi wa asili ya Makonde kama kabila la 43. Wananchi hao walio na makao yao kaunti ya Kwale watashiriki uchaguzi wa Agosti nane.

Show More

Related Articles