HabariMilele FmSwahili

Hali ya taharuki yatanda Baragoi baada ya watu 3 kuuawa na wezi wa mifugo

 

Hali ya taharuki ingali imetanda huko Baragoi kaunti ya Samburu badaa ya watu watatu kuuwawa na wezi wa mifugo usiku wa kuamkia leo. Afisa wa polisi ni miongoni mwa watu watatu waliojeruhiwa vibaya kwenye shambulizi hilo.Mshirikishi wa serikali kuu kanda ya bonde la ufa Wanyama Musyambo amedhibitisha shambulizi hilo akisema wezi waliojihami waliwavamia wafugaji waliokua wanatoka malishoni na kuanza kuwashambulia kabla ya kutoroka na idadi ya mifugo isiojulikana. Hata hivyo mifugo hao walirejeshwa na polisi waliokua wanashika doria eneo la kambi Nyoka huku akisema msako mkali kuwasaka wezi hao unaendelea. Aidha wenyeji wanaiomba serikali kuimarisha usalama eneo hilo.

Show More

Related Articles