HabariMilele FmSwahili

Bethuel Kiplagat kuzikwa leo

Aliyekua mwenyekiti wa tume ya haki,ukweli na maridhiano(TJRC) Bethuel Kiplagat anazikwa leo nyumbani kwake kaunti ya Nandi. Kiplagat alifariki wiki jana alipokua anapokea matibabu katika hosiptali ya Nairobi akiwa na miaka 82. Japo kulikua na taraifa kwamba rais Uhuru Kenyatta angekua miongoni mwa viongozi waliotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ya mazishi,haijabainika iwapo ataweza kuhudhuria. Mbali na kuhudumu kama mwenyekiti wa TJRC, Kiplagat alihudumu kama balozi wa kenya nchini ufaransa na uingereza na pia kuhudumu kama katibu katika wizara ya mambo ya nje wakati wa utawala wa rais mstafau Daniel moi.

Show More

Related Articles