HabariMilele FmSwahili

IEBC kufutilia mbali kampeini za wagombea 2 wa ugavana UasinGishu iwapo hawatadhibiti wafuasi wao

Tume ya uchaguzi IEBC imeonya kwamba huenda ikalazimika kufutilia mbali kampeni za wagombea wawili wa ugavana kaunti ya Uasin Gishu iwapo hawatawadhibiti wafuasi wao dhidi ya kushambuliana kila mara. Afisa mkuu wa IEBC  kanda ya kaskazini mwa bonde  la ufa  Jackton Nyonje anasema atawaagiza gavana Jackson Mandago na mpinzani wake   Zedekiah Buzeki kufika mbele ya tume hiyo kuelezea kuhusu vurugu zilizoshuhudiwa jana kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yao. Anasema idara za usalama zikishirikiana na IEBC zinendesha uchunguzi wake  kufuatia vurugu  hizo na iwapo  watapatikana kukiuka sheria  za  uchagizi   watakabiliwa vilivyo.Haya yanajiri baada ya watu saba kujeruhiwa jana usiku pale wafuasi wa wagombea hao walipokabiliana kati kati mwa mji wa Eldoret ambapo wanaendelea kupokea matibabu. Ni makabiliano ambayo yamelaaniwa vikali na viongozi wa kidini kaunti hiyo wakiongozwa na askofu wa kanisa katoliki Cornelius Korir na mwenyekiti wa baraza la maimamu na wahubiri Abubakar bin.

Show More

Related Articles