HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta akanusha madai yakutumia jeshi kuhitilafyana na uchaguzi

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamepuzilia mbali madai ya kutumia jeshi kuhitilafyana na uchaguzi mkuu. Wakiwhautubia wenyeji eneo la Kasarani hapa Nairobi,rais na naibu wkae wamesema lengo lao ni kushinda uchaguzi ulio huru na haki. Viongozi hao wanasema wapinzani wao wanaoeneza uvumi huo wameona watashindwa hivyo sasa lengo lao ni kuwachochea wakenya. Rais na naibu wake wamewataka wana NASA kukoma kutumia mahakama kupata uongozi badala yake kuuza sera zao kwa wakenya. Wamesisitiza uchaguzi utaandaliwa Agosti nane kinyume na shinikizo za upinzani kutaka uhairishwe.

Show More

Related Articles