HabariMilele FmSwahili

Marekani kupiga marufuku raia wake kusafiri Korea Kaskazini

Marekani inapanga kupiga marufuku raia wake wasisafiri kwenda Korea Kaskazini, kwa mujibu wa mashirika mawili ya kupanga safari ambayo yanafanya kazi humo. Mashirika hayo ya Koryo tours na Young Pioneer tours yamesema marufuku hiyo itatangazwa tarehe 27 Julai na itaanza kutekelezwa siku 30 baadaye. Hata hivyo serikali ya marekani bado haijathibitisha taarifa hizo. Young Pioneer Tours ndio waliofanikisha mwanafunzi mmarekani Otto Warmbier kuzuru Korea Kaskazini. Alikamatwa baadaye muda mfupi kabla yake kuondoka nchini humo na akahukumiwa kufungwa jela miaka 15. Hata hivyo, alirejeshwa marekani mwezi juni akiwa amepoteza fahamu na akafariki dunia wiki moja baadaye.kampuni hiyo, yenye makao yake China, imesema haitasaidia wamarekani wengine kuingia Korea Kaskazini.

Show More

Related Articles