HabariMilele FmSwahili

Chakula kilichosababisha kipindupindu KICC hakikuandaliwa na hoteli ya San Valencia

Chakula kinachodaiwa kusababisha maradhi ya kipindu pindu kwa wageni waliokua wanahudhuria kongamano la kimataifa katika jumba la KICC hakikuandaliwa na hotel ya San Valencia. Haya ni kulingana na afisa mkuu wa hoteli hiyo Phineas Kimathi ambaye anasema uchunguzi umeonyesha chakula hicho kiluka salama. Katika taarifa,Kimathi anasema siku ambayo walisambaza chakula kwa wageni huko KICC, chakula hicho pia kilisambazwa kwa wageni walio kua wanahudhuria mikutano maeneo tofauti na hadi leo hakuna lalama zimewasilishwa kutoka kwa mikutano hiyo tofauti. Japo amepongeza uchunguzi ambao umekua ukiendeshwa na maafisa wa afya kutoka wizara ya afya, amelalamikia hatua ya kufungwa kwa biashara yao akisema imewasababishia hasara kubwa na kusisitiza kwamba wanazingatia usafi wanapoandaa vyakula hotelini humo.

Show More

Related Articles