HabariMilele FmSwahili

Jubilee kupeleka kampeini zake kaunti ya Mandera na Wajir

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William ruto wnaapeleka kampeini za kujipigia debe kaunti za Mandera na Wajir leo. Rais na naibu wake wameratibiwa kuanza ziara yao Mandera ambapo watahutubia mikutano ya kisiasa huko Elwak na Mandera mjini mtawalia. Kisha baadaye viongozi hao watafululiza hadi Wajir ambapo watawahutubia wenyeji huko habaweni kisha baadaye Wajir mjini. Rais na naibu wake wanaelekea kaunti hizo badaa ya kupiga kambi Nairobi hapo jana mabapo waliwakashifu wapinzani wao kwa kueneza propaganda kwamba wanataka kutumia jeshi kusalia mamlakani.

Show More

Related Articles