HabariMilele FmSwahili

Wafuasi 7 wa Buzeki wajeruhiwa baada ya makabiliano na wafuasi wa Mandago

Watu saba wanaodaiwa kuwa wafuasi wa mwaniaji kiti cha ugavana kaunti ya Uasin Gishu Zedekiah Buzeki wanapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Moi wakiwa na majeraha mabaya baada yao kukabiliana na wafuasi wa gavana Jackson Mandago hapo jana jioni. OCPD wa Eldoret mjini Samuel Mutunga  amesema mamia ya wafuasi walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe ambapo wengine walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Anasema uchunguzi unaendeshwa kuwasaka waliohusika katika ghasia hizo ambapo Buzeki aliponea chupuchupu kujeruhiwa na wafuasi wa gavana Mandago waliokatiza msafara wake wa siasa uliokuwa ukielekea katikati mwa mji wa Eldoret. Ni vurugu zilizowalazimisha polisi kutumia vitoa machozi kuwatawanya wafuasi hao waliokabiliana kwa dakika kadhaa.

Show More

Related Articles