HabariMilele FmSwahili

Peter Munya na Ongwae wa Kisii wanaongoza kwa umaarufu

Magavana Peter munya wa Meru, James Ongwae wa Kisii na David Nkedienye wa Kajiado wangechaguliwa leo endapo uchaguzi ungeandaliwa. Haya ni kwa mujibu wa kura ya maoni iliyotolewa na INFOTRAK.Kaunti ya Meru, Munya wa PNU amepata uungwaji mkono wa asilimia 42 dhidi ya asilimia 40 za seneta Kiraitu Murungi ambaye anawania kupitia Jubilee. Kaunti ya Kajiado gavana David Ole Nkedienye wa ODM alipata uungwaji mkono wa asilimia 52 dhidi ya Jospeh Ole Lenku wa Jubilee aliyepta asilimia 41. Gavana James Ongwae wa ODM naye amepata uungwaji mkono wa asilimia 60 dhidi asilimia 16 wanaomuunga Chris Obure wa Jubilee.

Show More

Related Articles