HabariMilele FmSwahili

Takriban wakenya 1,200 wanaugua maradhi ya kipindupindu

Takriban wakenya 1,200 kote nchini wanaugua maradhi ya kipindupindu. Shirika la msalaba mwekundu linasema idadi hiyo huenda ikaongeza iwapo hatua mahususi hazitachukuliwa. Katibu mkuu wa shirika hilo Abbas Gullet anasema, shirika hilo linalenga kujenga zaidi ya vituo 6 vya kutoa matibabu kwa waathiriwa wa ugonjwa huo hasaa katika mitaa ya mabanda hapa Nairobi kuzuia kuenea ugonjwa huo. Anasema Nairobi na Gairsa ni baadhi ya kaunti zilizathirika zaidi na ugonjwa huo

Show More

Related Articles