HabariMilele FmSwahili

Visa vya ugonjwa wa Malaria vyaongezeka Pokot Magharibi

Wizara ya afya imedhibitisha kuongezeka visa vya ugonjwa wa Malaria katika kaunti ya Pokot Magharibi kutokana na mvua kubwa inayonyesha kaunti hiyo. Wizara hiyo imesema asilimia 16 ya wagonjwa wengi wao watoto wanaotafuta matibabu katika hospitali ya Kapenguria wanaugua ugonjwa huo. Ofisa mkuu wa afya na usafi kaunti hiyo Christine Akuto  ameonya kuwa viwango zaidi vitashuhudiwa huku mvua ikiendeea kunyesha. Akuto anasema visa vingi vya ugonjwa huo pia vimeripotiwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Amewataka wakazi kufafuta matibabu ya dharura wanapohisi dalili za Malaria. Pia ametoa wito kwa serikali kuu kusuluhisha upesi mgogoro wa wauguzi wanaogoma akisema hali hiyo inaathiria huduma kwa wagonjwa.

Show More

Related Articles