MichezoMilele FmSwahili

Starlets Junior kugaragaza dhidi ya Botswana

Timu ya taifa ya kandanda akina dada kwa chipukizi wasiozidi miaka 20 inamenyana na Botswana hii leo  kwenye ngarambe ya ufunguzi ya kusaka nafasi ya kushiriki kombe la dunia mwaka wa 2018.

Kikosi hicho cha chipukizi 20 walioteuliwa baada ya mashindano  ya shule za upili kiliondoka humu siku ya Jumatano asubuhi huku vipusa hao wakilenga kuwa miongoni mwa timu mbili zitakazowakilisha bara afrika.

Iwapo vipusa hao wa nyumbani watazoa ushindi hii leo  watakutana na Ethiopia kwenye mchuano wa raundi ya kwanza September tarehe 15.

Mchuano wa marudiano baina ya starlets junior na Botswana utasakatwa agosti nne humu nchini.

Show More

Related Articles