HabariPilipili FmPilipili FM News

Basi La Shule Lamuua Mwanafunzi Mombasa.

Mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi ya St.Augastine amefariki mapema leo baada ya kuhusika kwenye ajali eneo la Tononoka hapa Mombasa.

Inaarifiwa mwanafunzi huyo amefariki baada ya kukanyagwa na basi la shule hiyo wakati wakipelekwa shuleni.

Hii ni baada ya mwanafunzi huyo kuanguka barabarani kutoka kwa basi hilo ,kupitia sehemu ya chini ya basi iliyotoboka kutokana na kutu.

Walioshuhudia wanasema mwanafunzi huyo alikuwa anajaribu kuokoa chupa yake ya maji pamoja na bagi yake iliyoanguka kupitia mashimo yalioko ndani ya basi hilo.

Show More

Related Articles