HabariPilipili FmPilipili FM News

Achana Na Viongozi Wafisadi Sarai Amwambia Raila.

Mwaniaji wa kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa kwa tiketi ya chama cha WIPER Hassan  Omar Sarai amemtaka kinara mkuu wa CORD Raila Odinga kuachana na viongozi wafisadi hasa magavana  iwapo anataka kuwa kiongozi wa busara .

Akizungumza wakati wa kuzindua manifesto yake Sarai amedai kuwa Raila lazima amuunge mkono yeye kama gavana, kwani hana kashfa yoyote inayomkabili ikilinganishwa na gavana alieko mamlakani kwa sasa.

Sarai anasema kwa sasa kaunti ya Mombasa imekosa mwelekeo huku wananchi wengi walala hoi wakiendelea kudhulumika.

Katika mpango wake wa uongozi Sarai anadai manifesto yake imeangazia namna ya kukabiliana na ufisadi,kuipa kipau mbele miundo msingi, kuondoa kodi zote zisizokuwa na msingi sawia na kuhakikisha kuwa mji wa Mombasa una viwanda vya kutosha.

 

 

Show More

Related Articles