HabariPilipili FmPilipili FM News

Gavana Joho Afika Mahakamani.

Serikali ina nia yakunizuia kutetea kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa kupitia kesi ya stakabdhi zangu za masomo.

Gavana Hassan Joho ameiambia mahakama ya Mombasa.

Kupitia wakili wake James Orengo gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Ali Joho ameiambia mahakama kuwa serikali ina nia yakumuondoa mamlakani na kumuzuilia kutetea kiti chake cha ugavana.

Kupitia wakili James Orengo amesistiza kesi ambayo iko mahakamani dhidi ya Joho si kesi mpya bali ni sawa na kesi iliyowasilishwa na Janet Mbete mwaka 2013 ambayo awali mahakama iliitupiliwa mbali.

Wakili Orengo ameelezea mahakama kuwa ushahidi uliopo ni dhihirisho tosha kuwa kesi hiyo ina msukumo wa serikali na inanuia kumuadhibu mteja wake kutokana na msimamo wake wa kisiasa.

 

Show More

Related Articles