HabariPilipili FmPilipili FM News

IDPs Mombasa Bado Wangoja Fidia Kwa Serikali.

Waathiriwa wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 hapa Mombasa wameonekana kuzidi kulalamika kwa kukosa kufidiwa na serekali ya kitaifa baada ya kufurushwa kwenye makaazi yao..

Wakiongonzwa na wawakilishi wao Magdaline Kinyanjui na John Githinji,wamemtaka rais uhuru Kenyatta kuwapatia haki yao wakidai kwamba wamesaulika huku wenzao wakizidi kunufaika na pesa za kujiendeleza kimaisha kutoka serikalini.

Aidha Wamemtaka rais uhuru Kenyatta kuwaelezea mipango aliyonayo kuwahusu wakidai kuwa wao ni wafuasi suguu wa chamaa cha jubilee ambao wako tayari kumpigia kura kwenye uchaguzi mkuu ujao.

 

Show More

Related Articles