HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Watakiwa Kuwa Mabalozi Wa Amani.

Vijana wametakiwa kuwa mabalozi  wa Amani mitaani mwao wakati huu wa joto la siasa  na kukataaa kutumiwa na wanasiasa.

Hii ni mujibu wa kamishina wa kaunti ya Mombasa Evance Achoki aliyesema vijana wananafasi ya kulindaa mitaa yao na kudumisha amani mitaani mwao.

Achoki aidha amewataka vijana kuwekeza ujana wao katika masomo ya kitaaluma ili kujitaftia maisha kupitia njia halali.

Hata hivyo vijana wamelalamikia kutengwa na serikali za kaunti ya hata ile ya kitaifa huku hata wakiyalaumu mashirika ya serikali kwa kutozingatia maswala muhumu  ya kuwakwamua vijana kutoja kwa majanga ya kitaifa.

Show More

Related Articles