Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Odinga adai maafisa 42 wa usalama wanatumiwa kuiba kura

Mgombeaji urais wa muungano wa NASA Raila Odinga ameibua madai kwamba ana ujumbe kuwa kunao maafisa wa kusimamia uchaguzi 42 walioandikishwa ili kuvuruga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti nane.
Raila anasema upinzani ungali na ripoti za mkao wa mwezi Juni ulioashiria kwamba kura ya maoni iliyofadhiliwa na kikosi cha ujasusi iliashiria ushindi wa nasa wa hadi asilimia sabini.
Hata hivyo, rais Uhuru Kenyatta kwenye mkutano na ujumbe wa tume ya umoja wa Afrika ameusuta upinzani akisema kwamba unalenga kuzua machafuko na kulazimisha uchaguzi mkuu kuahirishwa.

Show More

Related Articles