HabariMilele FmSwahili

AU yaelezea kuridhishwa na maandalizi ya uchaguzi wa Agosti 8

Muungano wa Afrika AU umeelezea kuridhishwa na maandalizi ya taifa kwa ajili ya uchaguzi wa Agosti nane. Akizungumza baada ya kuongoza ujumbe wa viongozi kutoka muugano huo kukutana na kushauriana na washirika wa uchaguzi huo akiwemo rais Uhuru Kenyatta, mpinzani wake Raila Odinga, waakilishi wa idara ya mahakama na wakuu wa tume ya uchaguzi, mwenyekiti wa muungano huo Moussa Faki aliwarai wanasiasa kutekeleza kikamilifu mikataba ya amani waliosaini. Muungano huo umewatuma wajumbe wake nchini wakiongozwa na aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thambo Mbeki kufuatilia uchaguzi huo.

Show More

Related Articles