Elections 2017HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Mahakama ya Rufaa yaruhusu Al Ghurair ichapishe kura za urais

Ni rasmi sasa kampuni ya Al ghurair itaendelea kuchapisha karatasi za kura za urais, baada ya mahakama ya rufaa kubatilisha uamuzi wa mahakama kuu uliokuwa umeizuia kuendelea na zoezi hilo.
Katika uamuzi wa majaji watano wa mahakama ya rufaa, majaji hao wamesisitiza kuwa mahakama ilikosea iliposema kuwa wananchi walifaa kushirikishwa katika uamuzi wa kutoa kandarasi hiyo ya shilingi bilioni 2.5 kwa Alghurair.
Aidha mahakama hiyo ilikubaliana na uamuzi wa mahakama kuu kwamba hakukuwa na ushahidi kuonyesha Al ghurair ilikuwa na uhusiano na rais Uhuru Kenyatta.

Show More

Related Articles